
Jina lake ni Mercy. Kwa sasa ni mfanyabiashara kijana anayeendesha gari la kifahari aina ya Range Rover mitaa ya Nairobi, lakini nyuma ya mafanikio hayo kuna simulizi ya mateso na machozi.
Alipokuwa na umri wa miaka kumi na tano, maisha yake yalibadilika ghafla baada ya kupoteza wazazi wote wawili kwenye ajali ya barabarani. Bila msaada wa familia, aliishia mitaani.
Usiku wake mwingi aliutumia kulala kwenye vibanda vya carton, mara nyingine akipitia njaa kali. Ili kuishi, alisafisha viatu vya watu mjini na kutegemea shilingi chache zilizotokana na hiyo kazi ndogo ndogo.
Mercy alikua akiwa na ndoto kubwa, lakini alidharauwa na jamii. Watu walimwona kama msichana wa mtaa asiye na maana yoyote.
Aliamini siku moja maisha yake yangekuwa tofauti, lakini kila alipojaribu kubadili hali yake, mambo yalikuwa yanakwama. Alipojaribu biashara, haikufaulu. Alipojaribu kutafuta kazi ya heshima, hakupata nafasi. Ilionekana kana kwamba dunia nzima imefungia milango yake.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!