Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mwimbaji wa Injili Adaiwa Kutekwa Geita, Polisi Waanza Uchunguzi

  • 1
Scroll Down To Discover

Jeshi la Polisi mkoani Geita limeanza uchunguzi wa kina kufuatia taarifa za kutoweka kwa mwimbaji wa nyimbo za injili, Elisha Juma, mkazi wa Mtaa wa Kadisi, Kata ya Katente, Tarafa ya Ushirombo, Wilaya ya Bukombe.

Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na polisi, Elisha alichukuliwa na watu watatu wasiojulikana waliokuwa wakitumia gari jeupe lisilojulikana usajili wake. Tukio hilo lilitokea majira ya saa 10:00 jioni katika studio ya MAS J iliyopo Mtaa wa Kilimahewa, Kata ya Bulangwa.

Mashuhuda waliokuwepo eneo la tukio walieleza kuwa watekaji walifika kwa kasi, kumchukua mwimbaji huyo na kuondoka naye kusikojulikana, bila kutoa nafasi ya msaada. Hata hivyo, hawakuwasilisha taarifa mara moja kwa mamlaka husika hadi baadaye walipoelekeza taarifa Kituo cha Polisi Bukombe.

Akizungumza kuhusu tukio hilo, msemaji wa Jeshi la Polisi mkoani Geita amethibitisha uchunguzi unaendelea:

“Ni kweli tumepokea taarifa za kutoweka kwa kijana huyu na uchunguzi wa kina umeanza mara moja ili kubaini alipo na waliomchukua. Tunawataka wananchi kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola ili kufanikisha upatikanaji wa taarifa sahihi.”

Jeshi la Polisi limewataka wananchi kuwa watulivu na kuepuka kusambaza taarifa zisizo rasmi mitandaoni, huku likiahidi kutoa taarifa zaidi kadri uchunguzi utakavyosonga mbele.



Prev Post Zawadi Za Kwenye Chama Zapigwa  Marufuku Zanzibar 
Next Post Rigathi Gachagua Arejea Kenya Baada ya ziara Marekani
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook