Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limeeleza kuwa linaendelea na uchunguzi wa tukio la mauaji ya mwanamke aliyefahamika kwa jina la Humphrey Elisamon, maarufu kama Msoka, mwenye umri wa miaka 63, anayedaiwa kuuawa na mumewe kwa kutumia panga.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi Dar es Salaam Oktoba 19, 2026, tukio hilo lilitokea Oktoba 18, 2026, eneo la Mtaa wa Mungu Mwema, Hongoro Kibamba, jijini Dar es Salaam.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa mtuhumiwa wa mauaji hayo ni Dickson Elimringi Msoka, mwenye umri wa miaka 22, ambaye ni mtoto wa marehemu wa kambo.
Inadaiwa kuwa mwanamke huyo aliuawa baada ya kushambuliwa kwa panga kichwani. Hata hivyo, mtuhumiwa naye alishambuliwa na wananchi kabla ya polisi kufika eneo la tukio, akiwa katika hali mbaya. Baadaye alipelekwa hospitalini kwa ajili ya matibabu.
Jeshi la Polisi limesema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea ili kubaini mazingira kamili ya mauaji hayo.
Katika taarifa hiyo, Polisi Dar es Salaam imewataka wananchi kuendelea kushirikiana na mamlaka za serikali za mitaa, viongozi wa dini na wadau wengine katika kutatua changamoto za kijamii, kiuchumi, kisheria na kidini kwa njia zinazofaa, badala ya kuchukua hatua zinazoweza kusababisha madhara makubwa.
Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi Dar es Salaam.

The post Polisi Watoa Taarifa Mauaji ya Mwanamke wa Miaka 63 Kibamba appeared first on Global Publishers.











Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!