Kenya imethibitisha kisa cha tatu cha ugonjwa wa Ebola baada ya mwanamke mwenye umri wa miaka 65, ambaye alikuwa amewekwa karantini kutokana na kukaribiana na wagonjwa wawili wa kwanza, kubainika kuambukizwa virusi vya ugonjwa huo. Kwa mujibu wa Wizara ya Afya, mwanamke huyo, ambaye ni ndugu wa karibu wa wagonjwa hao wawili, alipata homa, maumivu ya koo na udhaifu wa mwili akiwa bado chini ya uangalizi wa afya. Baada ya kutengwa kwa ajili ya matibabu, alifanyiwa vipimo vilivyothibitisha kuwa ameambukizwa virusi vya Ebola aina ya Bundibugyo.
#Ebola #Kenya #bbcswahili #bbcswahilileo #bbcdirayadunia
Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw









Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!