Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Polisi Njombe Yachunguza Askari Anayedaiwa Kumshambulia Dereva Wa Lori

  • 28
Scroll Down To Discover

Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe limeanza kuchunguza tukio la askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani anayesambaa kwenye mitandao ya kijamii akionekana kumshambulia dereva wa gari kubwa aina ya lori.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe Oktoba 5, 2026, uchunguzi huo unaendelea sambamba na utekelezaji wa majukumu ya jeshi hilo kwa kuzingatia misingi ya kisheria na kuwachukulia hatua wahalifu wote wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu kwa kushirikiana na wananchi na vyombo vilivyo kwenye Mnyororo wa Haki Jinai.

Aidha, Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe limetoa wito kwa wananchi wote kuzingatia sheria na kujiepusha na vitendo vya kihalifu, likisisitiza kuwa halitakuwa na muhali kwa yeyote atakayebainika kutenda matukio ya uhalifu.

The post Polisi Njombe Yachunguza Askari Anayedaiwa Kumshambulia Dereva Wa Lori appeared first on Global Publishers.



Prev Post Chivayo na Mkewe Kuzikwa Bila Vichwa, Familia Yafichua Kilichopatikana
Next Post Ukikosa Namba Zote Usikate Tamaa, Lucky Loser Bado Inakupa Nafasi
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook