Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Tanzania Yatikisa Miss Grand International, Yaingia Top 3

  • 12
Scroll Down To Discover

Miss Grand wa Tanzania, Jihan Mohin Dimack amefanikiwa kuingia kwenye Top 3 ya mashindano ya Country’s Power of the Year – Round 3, baada ya kupata kura na alama za juu katika mchakato wa upigaji kura uliofanyika kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa Miss Grand International.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Miss Grand International usiku wa leo Oktoba 4, 2026 kura hizo zilikusanywa kuanzia Oktoba 2 hadi 4, ambapo Miss Grand wa Tanzania  aliingia kwenye orodha ya washiriki watatu walioongoza kwa kupata jumla ya alama za juu.

Washiriki wengine walioingia hatua hiyo ni Miss Grand Ecuador na Miss Grand Vietnam.

Matokeo hayo pia yamejumuisha kura na sapoti ya ziada iliyokusanywa kupitia akaunti ya Instagram ya Mr. Nawat, ambayo ilizingatiwa katika tathmini ya raundi hiyo.

Miss Grand International imewapongeza washiriki hao watatu pamoja na mashabiki wao kwa sapoti kubwa waliyoendelea kuonyesha.

Hata hivyo, safari bado haijaisha.

Katika raundi inayofuata, ni washiriki wawili pekee watakaofanikiwa kusonga mbele hadi hatua ya mwisho ya kuwania taji la Country’s Power of the Year.

Mshindi wa taji hilo pia atapata nafasi ya moja kwa moja kwenye TOP 20 ya Grand Final.

Kwa sasa, macho ya mashabiki wa Tanzania yanaelekezwa kwa Miss Grand wa Tanzania, huku Watanzania wakihimizwa kuendelea kuonyesha nguvu na sapoti yao katika raundi hii inayofuata.

Tanzania iko Top 3 — sasa ni wakati wa kuonyesha “COUNTRY’S POWER”! 🇹🇿🔥

The post Tanzania Yatikisa Miss Grand International, Yaingia Top 3 appeared first on Global Publishers.



Prev Post Gachagua Aibua Tuhuma za Trilioni 28 Kati ya Ruto na Chivayo
Next Post Fahamu Sababu Zinazofanya Mapera Kuwa Miongoni mwa Matunda Bora
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook