Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Maganya Awataka Wakosoaji wa Serikali Kutembelea Miradi ya Maendeleo – Video

  • 4
Scroll Down To Discover

MANYARA — Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Fadhili Maganya, amewataka baadhi ya wanasiasa wanaoikosoa Serikali kutembelea maeneo mbalimbali nchini ili kujionea utekelezaji wa miradi ya maendeleo na maboresho yanayofanyika katika huduma kwa wananchi.

Maganya ameyasema hayo Oktoba 4, 2026, wakati akiendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Manyara, akiongozana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Manyara, Janes Darabe.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Fadhili Maganya.

Katika ziara hiyo iliyofanyika Wilaya ya Mbulu, Maganya amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wanachama wa Jumuiya ya Wazazi.

Amesema ziara za kutembelea maeneo mbalimbali nchini zinasaidia viongozi na wadau kuona kwa uhalisia namna miradi ya maendeleo inavyotekelezwa na huduma zinavyoboreshwa kwa wananchi.

Maganya amesisitiza umuhimu wa kupata taarifa za maendeleo kutoka maeneo husika badala ya kutegemea taarifa za pembeni wakati wa kutoa tathmini kuhusu utekelezaji wa shughuli za Serikali.

Ziara hiyo ni sehemu ya shughuli za Jumuiya ya Wazazi katika mkoa wa Manyara, ambapo viongozi wameendelea kufuatilia utekelezaji wa miradi na kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi na wanachama.

The post Maganya Awataka Wakosoaji wa Serikali Kutembelea Miradi ya Maendeleo – Video appeared first on Global Publishers.



Prev Post Mvuvi Akaa Siku 4 Baharini, Ashuhudia Wenzake Wakifa, Afunguka – Video
Next Post Chivayo na Mkewe Kuzikwa Oktoba 8 Makaburi ya Glen Forest, Harare
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook