Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Dkt. Mwigulu Akutana na Viongozi wa Madereva, Mgomo Wasitishwa

  • 9
Scroll Down To Discover

DAR ES SALAAM: Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa madereva wa mabasi na malori nchini, hatua iliyofuatia makubaliano ya kusitisha mgomo wa madereva uliodumu kwa siku mbili.

Mazungumzo hayo yamefanyika leo, Septemba 30, 2026, katika Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Baada ya mazungumzo hayo, viongozi wa madereva wamekubali kusitisha mgomo huo, hivyo kuwezesha huduma za usafiri kuendelea kama kawaida nchini.

Serikali pia imeeleza utayari wake wa kusikiliza na kufanyia kazi changamoto zinazowakabili madereva, kwa lengo la kutafuta suluhisho la masuala yaliyosababisha mgomo huo.

Hatua hiyo inatarajiwa kurejesha huduma za usafiri huku Serikali na wadau wa sekta ya usafirishaji wakiendelea na majadiliano kuhusu changamoto zinazowakabili madereva.

Makubaliano hayo yamekuja baada ya mgomo wa siku mbili ambao uliathiri huduma za usafiri katika maeneo mbalimbali nchini.

The post Dkt. Mwigulu Akutana na Viongozi wa Madereva, Mgomo Wasitishwa appeared first on Global Publishers.



Prev Post Mgomo wa Madereva: Katambi Aweka Wazi Hatua za Serikali, Leseni Zarejeshwa – Video
Next Post Urusi Yashambulia Miundombinu ya Nishati Ukraine, Watu Wanne Wauawa Kyiv
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook