Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Waziri Katambi Awasili Stendi ya Mbezi Magufuli Kufuatia Mgomo wa Madereva – Live

  • 7
Scroll Down To Discover


DAR ES SALAAM: Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amewasili katika Stendi Kuu ya Mabasi ya Mbezi Magufuli jijini Dar es Salaam, kufuatia kusitishwa kwa safari za mabasi kunakodaiwa kusababishwa na mgomo wa madereva.

Katambi amefika stendi hiyo jioni hii kwa ajili ya kukutana na madereva pamoja na abiria waliokwama kutokana na kusitishwa kwa safari za mabasi.

Waziri huyo anatarajiwa kuzungumza na madereva na abiria mbele ya vyombo vya habari, huku akieleza hatua zitakazochukuliwa kuhusu hali hiyo.

Mgomo huo umeathiri huduma za usafiri katika baadhi ya vituo vya mabasi nchini, huku madereva wakieleza kuwa wanapinga masuala mbalimbali yanayohusiana na adhabu na faini za usalama barabarani.

Hali hiyo imesababisha baadhi ya abiria kushindwa kuendelea na safari zao, huku mabasi yaliyokuwa yamepangwa kuondoka yakiwa hayajaanza safari.

The post Waziri Katambi Awasili Stendi ya Mbezi Magufuli Kufuatia Mgomo wa Madereva – Live appeared first on Global Publishers.



Prev Post Polisi wachunguza mauaji ya watu 27 Afrika Kusini. Katika Dira ya Dunia TV.
Next Post Video: DCEA Yakamata Mirungi na Bangi Zikisafirishwa kwa Mabasi na Magari
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook