Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Messi Afikisha Mabao 922, Historia Yazidi Kuandikwa Marekani

  • 4
Scroll Down To Discover

MIAMI, Marekani — Nyota wa Argentina, Lionel Messi, ameendelea kuweka historia katika soka baada ya kufikisha jumla ya mabao 922 katika maisha yake ya soka.

Messi alifikia idadi hiyo baada ya kufunga bao lake la 70 katika Ligi Kuu ya Marekani (MLS) akiwa na Inter Miami, katika mchezo uliomalizika kwa sare ya 2-2 dhidi ya Philadelphia Union.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 39 alifunga bao hilo dakika ya 60, likiwa moja ya mabao yaliyomsaidia kuendelea kuongeza rekodi zake katika soka la Marekani.

Bao hilo limeongeza rekodi ya Messi tangu alipohamia Inter Miami, ambapo ameendelea kuonyesha kiwango cha juu licha ya kuwa katika hatua ya mwisho ya safari yake ya soka.

Kwa kufikisha mabao 70 katika MLS, Messi anaendelea kuweka alama katika ligi hiyo na kuongeza idadi ya rekodi binafsi ambazo ameweka tangu kuanza kucheza soka la kulipwa.

Hata hivyo, bao hilo limekuja baada ya kipindi ambacho Messi amekuwa akikabiliwa na changamoto katika kiwango chake binafsi, lakini bado ameendelea kuwa miongoni mwa wachezaji wenye ushawishi mkubwa katika timu yake.

Messi ameendelea kuongeza idadi ya mabao katika kila hatua ya safari yake ya soka, akitengeneza rekodi ambazo zimekuwa sehemu ya mjadala mkubwa kuhusu nafasi yake miongoni mwa wachezaji bora zaidi kuwahi kucheza mchezo huo.

Kwa kufikisha mabao 922, macho ya mashabiki sasa yataendelea kuwa kwake kuona kama ataweza kuvuka hatua nyingine kubwa katika mbio zake za kuongeza idadi ya mabao kabla ya kutundika daruga.

Na Mputa Ngaga, GPL- TUDACO

The post Messi Afikisha Mabao 922, Historia Yazidi Kuandikwa Marekani appeared first on Global Publishers.



Prev Post Trump atishia vikwazo vya kiuchumi kwa nchi yoyote inayoisadia Iran. Katika Dira ya Dunia TV.
Next Post Miaka 11 Baada Ya Kustaafu, Ronaldinho Arejea Kwenye Soka
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook