Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Baba Mzazi wa Lionel Messi Jorge Azikwa Nchini Argentina

  • 15
Scroll Down To Discover

Baba mzazi wa  nyota wa kimataifa wa Argentina Lionel Messi, Jorge Messi amezikwa katika makaburi binafsi ya El Prado, karibu na mji wa Rosario katika mazishi yaliohudhuriwa na watu wachache, jumapili.

Messi anayecheza katika klabu ya  Inter Miami ya marekani alifika pamoja na mkewe Antonela Roccuzzo na watoto wake Jumamosi usiku kwa ndege binafsi ili kuungana na mama yake Celia Cuccittini na ndugu zake wakati wa mazishi.

 

Katika kuomboleza kifo chake Shirikisho la Mpira wa Miguu la Argentina (AFA), ilielekeza mechi zote za wikiendi kuanza kwa dakika moja ya ukimya kama heshima kwa Jorge Messi, na wachezaji, benchi la ufundi na kuvaa vitambaa vyeusi mikononi.

Jorge Messi alifariki mapema Jumamosi akiwa na umri wa miaka 68, baada ya kukaa hospitalini Sanatorio Centro de Rosario kutokana na matatizo ya kiafya yaliyotokana na ugonjwa wa muda mrefu.

Jorge alikuwa mtu muhimu sana katika safari ya Lionel Messi ya soka, hasa katika miaka yake ya mwanzo na katika kusimamia masuala yake ya soka.

Enzi za uhai wake alifanikisha uhamisho wa Lionel kutoka Barcelona kwenda Paris Saint German (PSG) na kutoka PSG kwenda Inter Miami ya Marekani.

 

The post Baba Mzazi wa Lionel Messi Jorge Azikwa Nchini Argentina appeared first on Global Publishers.



Prev Post Viongozi Wa Chadema, TLS Na ACT Wafika Mahakamani Kufuatilia Kesi Ya Lissu – Video
Next Post Rashford Arejea Manchester United Apewa Jezi namba 14
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook