Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Diddy Aongezewa Muda wa Kukaa Gerezani Baada ya Kuzua Ugomvi

  • 13
Scroll Down To Discover

Msanii na mfanyabiashara maarufu wa muziki Sean ‘Diddy’ Combs ataendelea kutumikia kifungo chake kwa muda mrefu zaidi baada ya mamlaka za magereza nchini Marekani kusogeza mbele tarehe yake ya kuachiliwa huru.

Kwa mujibu wa taarifa za Federal Bureau of Prisons, Diddy sasa anatarajiwa kuachiwa huru Februari 20, 2028, badala ya Januari 2028 kama ilivyokuwa imepangwa hivi karibuni.

Mabadiliko hayo yanakuja baada ya Diddy kuhusishwa na ugomvi uliotokea akiwa gerezani. Ingawa aliwahi kuwekwa kwenye kifungo cha upweke kufuatia tukio hilo, mamlaka hazijatoa maelezo rasmi kuhusu sababu ya kurejesha tena tarehe yake ya kuachiliwa hadi Februari.

Kwa kipindi cha miezi ya karibuni, tarehe ya kuachiliwa kwa Diddy imekuwa ikibadilishwa mara kadhaa. Awali ilikuwa imepangwa katikati ya mwaka, baadaye ikahamishwa Aprili, kisha Februari, ikasogezwa Januari, na sasa imerejeshwa tena Februari 2028.

Diddy anatumikia kifungo cha miezi 50 jela baada ya kutiwa hatiani mwezi Oktoba 2025 kwa makosa mawili yanayohusiana na usafirishaji wa watu kwa madhumuni ya ukahaba.

The post Diddy Aongezewa Muda wa Kukaa Gerezani Baada ya Kuzua Ugomvi appeared first on Global Publishers.



Prev Post Depú Akaribia Kuachana na Yanga? Petro de Luanda Yajitokeza
Next Post Uganda kutuma wanajeshi wake Gaza. Je, watafaulu kuleta amani? Katika Dira ya Dunia TV.
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook