Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Waziri wa Mambo ya Nje Iran Amjibu Rais wa Lebanon Kwa Maneno Makali

  • 12
Scroll Down To Discover

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi.

TEHRAN, Iran — Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, ametoa kauli kali akimjibu Rais wa Lebanon, Joseph Aoun, kufuatia ukosoaji wake dhidi ya Iran kuhusu madai ya kuingilia mambo ya ndani ya nchi hiyo.

Katika ujumbe wake aliouchapisha kwenye mtandao wa X siku ya Jumamosi, Araghchi alisema kuwa kauli za Rais Aoun zinaweza kuwafanya watu waamini kwamba Iran ndiyo inayohusika na uharibifu au mzozo unaoikumba Lebanon, akikanusha vikali tuhuma hizo.

Alikwenda mbali zaidi kwa kuishauri Lebanon ijilinde na adui wake wa kweli, akisisitiza kuwa matatizo ya nchi hiyo hayapaswi kuelekezwa kwa Iran.

Rais wa Lebanon, Joseph Aoun

Kauli hiyo imekuja kufuatia mahojiano ya Rais Joseph Aoun na CNN, ambapo aliitaka Iran kutoingilia masuala ya ndani ya Lebanon na kuheshimu mamlaka ya nchi hiyo.

Mvutano huu mpya unaongeza joto katika uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tehran na Beirut, ambao mara kwa mara umekuwa ukikumbwa na tofauti za kisiasa na kiusalama katika eneo la Mashariki ya Kati.

The post Waziri wa Mambo ya Nje Iran Amjibu Rais wa Lebanon Kwa Maneno Makali appeared first on Global Publishers.



Prev Post Rais Samia Aweka Rekodi ya Kupokea Shahada za Heshima Nyingi
Next Post Waziri Mkuu Aamuru Malipo ya Milioni 181 Kwa Mkazi wa Chunya
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook