
Kampuni ya mtandao wa simu ya Airtel Tanzania imekabidhi zawadi ya bajaji mpya kwa mshindi wa kampeni ya Mwaka Umenyooka na Airtel, Bw. Barnaba Dominick, mkazi wa Wilaya ya Babati mkoani Manyara, baada ya kujishindia kupitia matumizi ya huduma ya Airtel Money.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano hayo, Meneja wa Airtel Kanda ya Manyara, Kephar Kileo, amesema kuwa kampeni hiyo imelenga kuwazawadia wateja wanaotumia My Airtel App kufanya miamala yao ya kila siku, huku akibainisha kuwa wateja hao wamekuwa na nafasi kubwa ya kujishindia zawadi mbalimbali.
“Tunawapongeza wateja wetu kwa kuendelea kutumia huduma za Airtel, hususan My Airtel App. Kupitia kampeni ya Mwaka Umenyooka na Airtel, tumetoa zawadi mbalimbali ikiwemo pikipiki, magari, bajaji pamoja na fedha taslimu, kama njia ya kuthamini uaminifu wao,” alisema Kileo.
Kwa upande wake mshindi wa bajaji hiyo, Bw. Barnaba Dominick, ameonesha furaha yake kwa kushinda zawadi hiyo, akieleza kuwa itamsaidia kuboresha maisha yake kwa kuongeza kipato kupitia biashara ya usafirishaji wa abiria katika maeneo ya Babati.
“Nashukuru Airtel kwa zawadi hii kubwa. Bajaji hii itanisaidia kuanzisha na kukuza biashara yangu ya usafirishaji na hivyo kuongeza kipato changu na familia yangu,” alisema Dominick.
Aidha, amewahamasisha Watanzania wengine kuendelea kutumia My Airtel App kufanya miamala mbalimbali ili kupata nafasi ya kushinda zawadi zinazotolewa na Airtel Tanzania kupitia kampeni hiyo.
Airtel Tanzania inaendelea kujizatiti katika kutoa huduma bora za mawasiliano na kifedha pamoja na kuendesha kampeni bunifu zinazolenga kuwainua wateja wake kiuchumi.
The post Airtel Yampa Mkazi wa Babati Bajaji Mpya Kupitia Kampeni ya “Mwaka Umenyooka” appeared first on Global Publishers.











Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!