Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mtanzania Afariki Uturuki Baada ya Kudondoka Ghorofa ya 14, Utata Wazuka – Video

  • 9
Scroll Down To Discover

Kufuatia kusambaa kwa video mitandaoni ikimuonesha Mtanzania aliyefariki dunia baada ya kudondoka kutoka ghorofa ya 14 nchini Uturuki, umeibuka mjadala mkubwa kuhusu mazingira ya tukio hilo.

Baadhi ya taarifa zisizothibitishwa zimekuwa zikidai kuwa huenda bosi wa marehemu alihusika kwa kumsukuma kutoka juu ya jengo hilo.

Aidha, utata ulijitokeza kuhusu utambulisho wa marehemu baada ya picha mbili tofauti kusambazwa zikidaiwa kuwa ni za mtu huyo.

Akizungumzia sakata hilo, Mtanzania anayeishi nchini Uturuki na aliyewahi kuwa kiongozi wa diaspora ametoa ufafanuzi, akieleza kuwa marehemu ametambulika kwa jina la Martha Laurence Kiwanga, mkazi wa Tanga.

Ameongeza kuwa Mtanzania mwingine, Emiliana Leornald Nkya, ndiye aliyetoa taarifa ya tukio hilo kwa polisi na kwa sasa anashikiliwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Uchunguzi wa tukio hilo unaendelea, huku mamlaka husika zikitarajiwa kutoa taarifa rasmi zaidi.

The post Mtanzania Afariki Uturuki Baada ya Kudondoka Ghorofa ya 14, Utata Wazuka – Video appeared first on Global Publishers.



Prev Post BARKER AFICHUA SIRI YA MPANZU, DAKIKA ZA MWISHO
Next Post Chris Brown Azua Gumzo Baada ya Kumbusu Shabiki Jukwaani
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook