Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Viongozi wa Ulaya Walalamikia Vita vya Marekani na Israel Dhidi ya Iran

  • 10
Scroll Down To Discover

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, Yvette Cooper

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, Yvette Cooper amesema kuwa London haitajiunga katika vita vya Marekani na utawala wa wa Israel dhidi ya Iran.

Cooper amesisitiza kwamba London inajiepusha kuingia katika mzozo wa Magharibi mwa Asia. Amesema: “Tumepata funzo kutokana na vita vya Iraq na tutatumia uzoefu huo katika vita vya sasa.”

Wakati huo huo Sadiq Khan, Meya wa jiji la London amesema vita dhidi ya Iran bila ya mwafaka wa kimataifa haina idhini ya Umoja wa Mataifa; na Uingereza haipasi kuingia katika vita hivyo. Amesema, vita dhidi ya Iran huwenda vikatikisa pakubwa uchumi wa Uingereza.

Katika upande mwingine na katika kuendeleaa wimbi la upinzani wa kulaani vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran, Rais wa Jamhuri ya Ireland, Catherine Connolly amevitaja vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran kuwa ni jinai na kusisitiza kuwa, matukio ya hivi karibuni katika eneo la Magharibi mwa Asia ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa na hati ya Umoja wa Mataifa.

Naye Mary Robinson rais wa zamani wa Ireland ameituhumu serikali ya Donald Trump nchini Marekani kuwa inaeneza uongo.

Amesema: hivi sasa tunashuhudia vita vilivyoanzishwa na Israel na Marekani dhidi ya Iran na vita hivi vimesababisha uharibifu mkubwa katika eneo la Asia Magharibi.

Stori na Elvan Stambuli, Global Digital

RAIS TRUMP ATOA HOTUBA ya KIBABE – AJISIFIA KUIBOMOA IRAN KWA MAKOMBORA – VITA IPO PALEPALE

 

The post Viongozi wa Ulaya Walalamikia Vita vya Marekani na Israel Dhidi ya Iran appeared first on Global Publishers.



Prev Post Dkt. Mwigulu Aagiza Takukuru Kuchunguza Ujenzi Wa Hospitali Ya Wilaya Ya Kalambo
Next Post ALAF Yatoa Viti 10 vya Magurudumu kwa Watoto Wenye Mahitaji Maalumu
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook