Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mzee Bichuka Apokea Shilingi Milioni 10 Kutoka kwa Rais Samia Kupitia Naibu Waziri

  • 10
Scroll Down To Discover

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma, amemtembelea na kumjulia hali mwanamuziki nguli Mzee Hassan Rehani Bichuka nyumbani kwake Sinza Mori, jijini Dar es Salaam.

Mwinjuma alimtembelea mwanamuziki huyo Machi 9, 2026 na kufikisha salamu kutoka kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo alisema Rais Samia anamtakia Bichuka kila la heri na anamuombea afya njema ili apone haraka.

Naibu Waziri Mwinjuma alimkabidhi Mzee Bichuka shilingi milioni 10 taslimu, ikiwa ni mkono wa pole uliotolewa na Rais Samia kwa ajili ya kumtia moyo katika kipindi hiki cha matibabu.

The post Mzee Bichuka Apokea Shilingi Milioni 10 Kutoka kwa Rais Samia Kupitia Naibu Waziri appeared first on Global Publishers.



Prev Post MAJERUHI YAWALAZIMISHA PEDRO KUBADILI KIKOSI YANGA
Next Post Mo Dewji Atangazwa na Forbes Kuwa Tajiri Namba Moja Afrika Mashariki na Kati
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook