Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

MERIDIAN HOLDINGS INC KUWA UTAMBULISHO MPYA WA GOLDEN MATRIX GROUP

  • 24
Scroll Down To Discover

Kampuni ya kimataifa ya michezo ya kubashiri na burudani ya kidijitali, iliyokuwa ikijulikana kama Golden Matrix Group, sasa imeanza rasmi kutumia jina jipya la Meridian Holdings Inc.. Kuanzia leo, kampuni hii itafanya biashara katika soko la Nasdaq Capital Market kwa alama ya hisa MRDN. Hatua hii inalenga kuimarisha taswira yake ya kimataifa na kuendana na mwelekeo wa sasa wa biashara.

Mabadiliko haya yanakuja kama sehemu ya mkakati wa kuunganisha utambulisho wa kampuni na chapa yake kuu ya Meridianbet, ambayo imejijengea jina katika masoko mbalimbali duniani. Kupitia muundo wake mpya, Meridian Holdings Inc. sasa inasimamia taasisi sita muhimu ambazo ni Meridianbet, Expanse Studios, RKings, Classics for a Cause, GMAG na Mexplay.

Meridianbet haikuachi nyuma, kuna michezo mbalimbali ya kasino mtandaoni pamoja na mechi za kimataifa za kubashiri zenye odds bomba zinazokuongezea nafasi ya kuongeza kipato chako kila siku. Kujiunga ni rahisi! Tembelea meridianbet.co.tz au piga *149*10#.

Katika kuendeleza mkakati wake wa upanuzi, Meridianbet imefanikiwa kukamilisha ununuzi wa asilimia 100 wa Fairbet Ltd., kampuni ya michezo ya kubahatisha nchini Malta. Kupitia ununuzi huo, Meridianbet imeongeza kwa kiasi kikubwa wigo wa huduma zake katika maeneo ya Malta na Gozo. Hatua hii imeimarisha nafasi ya kampuni kama mtoa huduma na mwajiri muhimu katika soko hilo la Ulaya.

Aidha, Meridian Holdings Inc. inatarajia kutekeleza mpango wa kuunganisha hisa ili kuboresha muundo wa hisa zake sokoni. Lengo ni kuongeza ushindani wa hisa zake kwa wawekezaji wa taasisi na kupandisha thamani yake na viwango vya kimataifa vya sekta ya michezo ya kubahatisha.

Akizungumzia hatua hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu Zoran Milosevic ameeleza kuwa kuunganisha utambulisho wa kampuni ni sehemu ya safari ya mageuzi inayolenga kuongeza thamani kwa wanahisa na wadau wote. Alisisitiza kuwa mafanikio ya upanuzi nchini Malta yameipa kampuni ujasiri wa kuendelea kupanua uwepo wake kimataifa. Kwa mwelekeo huu mpya, Meridian Holdings Inc. inaingia katika sura mpya ya maendeleo na ushindani wa kimataifa.

The post MERIDIAN HOLDINGS INC KUWA UTAMBULISHO MPYA WA GOLDEN MATRIX GROUP appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA MGENI RASMI MAADHIMISHO YA SIKU YA MLAJI DUNIANI 2026
Next Post SINGIDA,TRA,PAMBA ZINACHANGAMOTO KUBWA SIMBA SC
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook