Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

BAADA YA KUPIGWA ‘STOP’ SINGIDA BS….AUCHO AVUNJA UKIMYA…’AMWAGA UGALI WOTE’….

  • 20
Scroll Down To Discover

KLABU ya Singida Black Stars SC imetangaza kumfungia miezi mitatu kiungo Khalid Aucho kwa kosa la utovu wa nidhamu na kuchelewa kazini.

Aidha, imemsimamisha kazi kipa Amas Obasogie kwa kipindi cha miezi mitatu ili kuruhusu uchunguzi wa tuhuma zinazohusiana na upangaji wa matokeo.

Kwa mujibu wa taarifa ya klabu hiyo iliyolewa leo na Ofisi ya Mtendaji Mkuu, kupitia Kamati ya Nidhamu, imewakumbusha wachezaji kuheshimu taratibu.

“Klabu inawakumbusha wachezaji na watumishi wake wote kuzingatia nidhamu, uwajibikaji na heshima kwa klabu,”imesema taarifa hiyo.

MWENYEWE AFUNGUKA..

KIUNGO wa Singida Black Stars, Khalid Aucho, amevunja ukimya kufuatia uamuzi wa klabu yake kumfungia kwa muda wa miezi mitatu kwa tuhuma za utovu wa nidhamu.

Kupitia ujumbe wake, Aucho ameeleza kuwa katika maisha yake yote ya soka amekuwa akijiheshimu na kuzingatia taaluma, akidai hajawahi kuhusishwa na tukio lolote la utovu wa nidhamu.

“Nimekuwa nikijibeba kwa weledi katika maisha yangu yote ya soka, nikiwakilisha kila klabu kwa heshima na nidhamu. Katika miaka yote niliyocheza mpira, sijawahi kuhusishwa na kesi yoyote ya utovu wa nidhamu kwa sababu ninaelewa wajibu unaokuja na kuwa mchezaji wa kulipwa,” ameeleza Aucho.

Nyota huyo raia wa Uganda ameongeza kuwa ana imani hali hiyo itapita na kurejea katika ubora wake, huku akitoa shukrani kwa mashabiki wanaoendelea kumuunga mkono katika kipindi hiki kigumu.

“Kwa mashabiki wangu wapendwa ambao mmekuwa nami wakati wote, hali hii itapita. Asanteni kwa msaada wenu endelevu,” ameongeza.

The post BAADA YA KUPIGWA ‘STOP’ SINGIDA BS….AUCHO AVUNJA UKIMYA…’AMWAGA UGALI WOTE’…. appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post KUELEKEA DABI YA KARIAKOO……YANGA MAPEMAAAA TU…..SHILINGI IKO JANGWANI KITAMBO….
Next Post 16 BORA ULAYA NI ‘UBAYA UBWELA’ MWANZO MWISHO….CITY vs MADRID, ARSENAL MCHEKEA…
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook