Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Simba Wa Vita Mzee Rashidi Mfaume Kawawa Ambaye Angekuwa Hai Jana Angetimiza Umri Wa Miaka 100

  • 12
Scroll Down To Discover

Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mzee Rashidi Mfaume Kawawa, mwanasiasa mashuhuri na mmoja wa viongozi waliokuwa karibu sans na xdwa Mwalimu Julius Nyerere katika harakati za uhuru na ujenzi wa taifa.

Mzee Kawawa aliyesaliwa tarehe 27 Februari 1926 na kufariki 31 Desemba 2009, alikuwa Waziri Mkuu wa pili wa Tanganyika kuanzia tarehe 22 Januari 1962 hadi 9 Desemba 1962, akichukua nafasi baada ya Julius Nyerere kujiuzulu kwa muda ili kuimarisha chama cha TANU.

Baada ya Tanganyika kupata uhuru kamili na kuwa Jamhuri, Mwalimu Nyerere alirejea madarakani kama Rais, ambspi baadaye Mzee Kawawa alikuja kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika muhula wa pili wa wadhifa huo kuanzia 17 Februari 1972 hadi 13 Februari 1977, alipomkabidhi madaraka marehemu Edward Moringe Sokoine. Kipindi hicho ndicho kilikuwa cha mwisho kuwepo kwa nafasi ya Waziri Mkuu kabla ya kurejeshwa tena mwaka 1984.

Mbali na uwaziri mkuu, Mzee Kawawa aliwahi kushika nyadhifa nyingi muhimu serikalini na katika chama cha TANU na baadaye CCM, na alijulikana kwa msimamo wake mkali wa nidhamu na uzalendo, jambo lililompatia jina la utani “Simba wa Vita.”

Anaendelea kukumbukwa kama mmoja wa viongozi wakuu waliotoa mchango mkubwa katika kupatikana kwa uhuru na ujenzi wa taifa la Tanzania.

The post Simba Wa Vita Mzee Rashidi Mfaume Kawawa Ambaye Angekuwa Hai Jana Angetimiza Umri Wa Miaka 100 appeared first on Global Publishers.



Prev Post Zanzibar kuchukua hatua za kisheria kwa meli iliyopatwa na dawa za kulevya, katika Dira ya Dunia TV
Next Post UAE Yasema Haitakaa Kimya Ikiwa Iran Itaendelea Kushambulia
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook