Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Kula Sahihi Wakati wa Ramadhani, Linda Afya Yako kwa Lishe Bora

  • 18
Scroll Down To Discover

 

Katika kipindi hichi cha Ramadhani na Kwaresima nataka kuwapa tips za vyakula ambavyo mnatakiwa kupika kipindi hiki.

Kama tunavyojua ukiwa katika swaumu lazima kuna baadhi ya vitamini vinaweza kupotea mwilini mwako, hivyo basi wapishi wa futari wanatakiwa kuzingatia mlo sahihi wakati wa kufungulia (kufuturu) ili kuendelea kuimarisha afya za walaji.

Mara nyingi vyakula vinavyoliwa kwa wakati huu ni aina ya mizizi kama vile mihongo, magimbi, viazi vitamu, vyakula ambavyo vyote vipo katika kundi la mlo mmoja, jambo ambalo halishauriwi kiafya.

Kwa mujibu wa Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC) vipo vyakula vinavyofaa na visivyofaa kuliwa wakati wa kufuturu katika msimu huu wa Ramadhan ikiwemo vyakula vyenye chumvi nyingi. Hivi havifai kwani vinaleta kiu na mwisho ukashindwa kufunga siku inayofuata.

Aina vya vyakula vinavyoshauriwa kuliwa/ kupikwa na kuliwa wakati wa kufuturu, kwanza hutakiwi kula vyakula vizito kwani vinaweza kukusababibisha kuumwa tumbo kutoka na kutokula chochote tangu asubuhi. Hivyo basi wapishi wa futari wanatakiwa kuacha kupika vyakula kwa mazoea kuwa futari lazima mihogo, viazi au magimbi.

Kinyume chake vipo vyakula vyepesi ambavyo vinafaa kuliwa na mfungaji ni vile vyepesi vikiwemo supu, mtori, mchemsho wa ndizi au samaki, na vingine ambavyo vya kawaida ikiwemo tambi, chapati za maji na viazi rosti au maini rosti. Kwa upande wa vinywaji kunywa uji, chai, juisi ya matunda, hasa yaliyosagwa nyumbani, kahawa, pamoja na maziwa.

Stori na Elvan Stambuli, Global Digital

The post Kula Sahihi Wakati wa Ramadhani, Linda Afya Yako kwa Lishe Bora appeared first on Global Publishers.



Prev Post Kamanda Muliro Atoa Onyo Kali Dhidi ya Uhalifu Dar, Ajibu Kuhusu Alipo Mafwele – Video
Next Post Ushuru mpya wa 10% wa Trump waanza kutekelezwa
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook