Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

SIMBA USHINDI WA KWANZA NYUMBANI

  • 32
Scroll Down To Discover

SIMBA imemaliza kibabe hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa kwa kupata ushindi wa hatua hiyo na wa kwanza pia nyumbani baada ya kuichapa Stade Malien kwa bao 1-0 nyumbani.

Ushindi huo umepatika kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa ikiwa ni mechi ya sita kwa kila timi katika Kundi D.

Mapema tu Simba ilianza pambano hilo kaa kasi na kuonyesha  pira biriani lililojengwa  na pasi za kutosha, na kufanikiwa kupata bao la kuongoza dakika ya pili tu kupitia kwa kiungo mshambuliaji, Anicet Oura.Bao hilo likauchangamsha zaidi mchezo huo, huku Simba ikitengeneza mashambulizi mengine  lakini mshambuliaji Seleman Mwalimu ‘Gomez’ na kiungo mshambuliaji Ellie Mpanzu walizipoteza nafasi kadhaa za kufunga.

Dakika ya 64 Simba ilifanya mabadiliko mawili pekee kwa kumtoa Elie Mpanzu na Alassine Cante na kumuingiza Morice Abraham na Loemba.

Malien iliwaka dakika ya 65 ikipoteza nafasi nzuri kupitia mshambuliaji, Taddeus Nkeng shuti lake likipanguliwa vyema na kipa wa SimbaDjibrilla Kasali aliyepata clean sheet ya kwanza michuano hiyo ya Caf tangu atue Msimbazi.

Licha ya ushindi huo, Simba imemaliza mkiani kwa kundi hilo ikiwa na pointi tano, nyuma ya Malien iliyoongoza kundi na pointi 11 ikifuatiwa na Esperance ya Tunisia iliyofikisha tisa baada ya usiku huu kuifunga Petro Atletico ya Angola iliyovuna alama sita na kushika nafasi ya tatu.

Malien na Esperance zimefuzu robo fainali zikiungana na Al Ahly, Al Hilal, Mamelodi na Pyramids kutoka makundi mengine hadi sasa.

Rasmi Simba inaelekeza nguvu kwenye michuano ya ndani, huku ikimaliza kibabe nyumbani kwa upande wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

The post SIMBA USHINDI WA KWANZA NYUMBANI appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post MCHAKATO UJENZI UWANJA WA YANGA WAFIKIA PATAMU
Next Post Rais Samia Awasili Zanzibar Baada ya Kushiriki Mkutano wa AU
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook