Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Rais Samia Awaapisha Viongozi Ikulu, Afafanua Sababu za Kumhamisha Waziri Salum (Picha +Video)

  • 23
Scroll Down To Discover

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali alipowaapisha, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 09 Februari, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Februari 09, 2026, amewaapisha viongozi mbalimbali aliowateua katika hafla iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam.
Miongoni mwa viongozi walioapishwa ni Waziri Salum, ambaye ameapa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara.

Akizungumza katika hafla hiyo, Rais Samia amegusia minong’ono iliyokuwepo miongoni mwa wananchi kufuatia uamuzi wake wa kumtoa Waziri Salum Ikulu, hatua iliyozua maswali kuhusu sababu ya mabadiliko hayo, ikizingatiwa kuwa wamefanya kazi kwa karibu kwa muda mrefu.

Rais Samia ameeleza kuwa mabadiliko anayoyafanya katika teuzi zake kwa viongozi aliowahi kufanya nao kazi yanalenga kuwakuza, kuwajengea uzoefu mpana wa uongozi na kuwaandaa kwa majukumu makubwa zaidi. Amefafanua kuwa hatakuwepo Ikulu milele, na kwamba viongozi watakaofuata wanaweza kuja na timu zao wenyewe, hivyo ni muhimu kwa viongozi wa sasa kupata fursa mbalimbali za kiuongozi mapema

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Balozi Waziri Rajab Salum kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 09 Februari, 2026.
Rais Dkt. Samia akimuapisha Kanali Yahya Ramadhani Kido kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
Rais Samia akimuapisha Meja Jenerali Marco Elisha Gaguti kuwa Balozi.

The post Rais Samia Awaapisha Viongozi Ikulu, Afafanua Sababu za Kumhamisha Waziri Salum (Picha +Video) appeared first on Global Publishers.



Prev Post Nafasi 99 za Ajira Serikalini
Next Post Video: Polisi Wanawatafuta Wanawake Waliompiga Mwenzao Kwa Mwiko
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook