Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mtoto wa Gaddafi Auwawa Kwa Shambulio na Watu Wenye Silaha Libya

  • 18
Scroll Down To Discover

Saif al-Islam Gaddafi, mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa Libya marehemu Kanali Muammar Gaddafi, ameripotiwa kuuawa kufuatia shambulio la ghafla la watu wenye silaha lililotokea magharibi mwa Libya siku ya Jumanne, kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa timu yake ya kisiasa.

Kwa mujibu wa Abdullah Othman Abdurrahim, mmoja wa wajumbe wa timu hiyo, watu wanne waliovalia barakoa na wakiwa na silaha walivamia makazi ya Saif al-Islam majira ya mchana katika mji wa Zintan. Washambuliaji hao wanadaiwa kutumia mbinu za hila kuingia ndani ya eneo hilo kabla ya kuzima kamera za ulinzi.

Taarifa zinaeleza kuwa baada ya kuzimwa kwa mifumo ya ufuatiliaji, kulitokea makabiliano ya moja kwa moja ya risasi kati ya walinzi na washambuliaji, hali iliyosababisha Saif al-Islam kupoteza maisha.

Baada ya tukio hilo, timu yake ya kisiasa imetoa wito kwa mamlaka za Libya pamoja na jumuiya ya kimataifa kufanya uchunguzi wa kina na wa haraka ili kubaini waliohusika na waliopanga shambulio hilo. Hata hivyo, hadi sasa, mamlaka za Tripoli na Zintan bado hazijatoa tamko rasmi kuthibitisha au kukanusha taarifa hizo.

Saif al-Islam alikuwa mmoja wa watu waliokuwa na ushawishi mkubwa lakini pia wenye mgawanyiko mkubwa kisiasa nchini Libya tangu mwaka 2011, wakati uasi ulioungwa mkono na NATO ulipoangusha utawala wa baba yake. Tangu wakati huo, amekuwa akihusishwa na juhudi za kurejea katika uongozi wa kisiasa huku akikabiliwa na upinzani mkali kutoka makundi mbalimbali ya kisiasa na kijeshi.

Iwapo taarifa hizi zitathibitishwa rasmi, kifo chake kinaweza kuongeza mvutano wa kisiasa na kiusalama nchini Libya, taifa ambalo bado linapambana na migogoro ya ndani na mgawanyiko wa madaraka.

MAREKANI YALIPUA DRONE ya IRAN KATIKA BAHARI ya UAJEMI SIKU CHACHE KABLA ya MAZUNGUMZO 📍USA

The post Mtoto wa Gaddafi Auwawa Kwa Shambulio na Watu Wenye Silaha Libya appeared first on Global Publishers.



Prev Post Ndege ya Iran Yadunguliwa na Jeshi la Marekani Karibu na Meli ya Kivita
Next Post Samsung Launches Galaxy Tab A11 in Tanzania, Expanding Access to Smart Learning and Everyday Entertainment
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook