Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Rita Norbert: Sioni Mwanamke Anayeweza Kunifunika Kwa Mvuto

  • 20
Scroll Down To Discover

Mwanadada Rita Norbert

Mwanadada Rita Norbert amezua mjadala mpana mitandaoni baada ya kudai kuwa, kwa hapa nchini, haoni mwanamke anayeweza kumfunika kwa mvuto wa kuvutia. Kauli hiyo imepokelewa kwa mitazamo tofauti, huku baadhi wakiiita ishara ya kujiamini, na wengine wakiona ni kauli ya kujitukuza kupita kiasi.

Rita, ambaye kwa nyakati tofauti amekuwa akivuta macho ya wengi kutokana na muonekano wake na mtindo wa maisha, anaonekana kusimama kwenye msimamo wake akiamini mvuto wake ni wa kipekee na hauwezi kulinganishwa kirahisi na wa wengine.

Hata hivyo, kauli hiyo imeibua kumbukumbu za nyuma pale Rita alipowahi kuhusishwa na madai ya kuvuruga uhusiano wa kimapenzi kati ya mastaa Zuchu na Diamond Platnumz. Ingawa suala hilo lilibaki kwenye fununu bila ushahidi wa wazi, bado jina lake limeendelea kutajwa kila panapozuka mjadala unaohusisha mahusiano ya mastaa hao.

The post Rita Norbert: Sioni Mwanamke Anayeweza Kunifunika Kwa Mvuto appeared first on Global Publishers.



Prev Post Mbwambo (34) Ajiua Kwa Kujikata Koromeo Akiwa Gesti – Video
Next Post Halmashauri ya Wilaya ya Songea Yatangaza Nafasi 5 za Ajira
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook