Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Bodi ya Ithibati kukagua waandishi wasio na sifa makazini

  • 121
Scroll Down To Discover

Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari imesema itaendesha ukaguzi maalumu katika vyombo vya habari na maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kujiridhisha kuwa watu wote wanaotekeleza majukumu ya kihabari wanakidhi vigezo vilivyoainishwa kwa mujibu wa sheria.

Bodi hiyo imesema imebaini kuwa kuna baadhi ya watu wasio na sifa wamerejea kutekeleza majukumu ya kihabari baada ya uchaguzi mkuu.

“Bodi inatoa onyo na kuwataka watu wote wanaofanya kazi za kihabari bila kuwa na ithibati kuacha mara moja, kwani kuendelea kufanya hivyo ni kosa kwa mujibu wa kifungu cha 50 (2) (b) cha sheria ya huduma za habari, sura ya 229,” imesema.

Aidha, bodi hiyo imesema haitasita kuchukua hatua stahiki za kisheria dhidi ya mtu au taasisi yoyote itakayobainika kuajiri au kuruhusu utekelezaji wa shughuli za kihabari bila kuzingatia utaratibu na masharti kwa mujibu wa sheria.

The post Bodi ya Ithibati kukagua waandishi wasio na sifa makazini appeared first on SwahiliTimes.



Prev Post CAMARA AIOKOA SIMBA, YAKATA TIKETI YA NUSU FAINALI
Next Post Nyota wa Ghana, Semenyo, Awa Mchezaji Aliyeuzwa Ghali zaidi Bournemouth
Related Posts
© Image Copyrights Title

Nafasi 53 za Ajira Serikalini

© Image Copyrights Title

Nafasi 50 za Ajira Serikalini

Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook