Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

MUKWALA AONGEZA NGUVU KUELEKEA NUSU FAINALI

  • 30
Scroll Down To Discover

MSHAMBULIAJI wa Simba, Steven Mukwala amerejea rasmi katika kikosi cha timu hiyo baada ya kumaliza majukumu yake na timu ya taifa ya Uganda iliyoshiriki Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025.

Mukwala alikuwa miongoni mwa wachezaji walioitwa kuunda kikosi cha Uganda kilichoshiriki michuano hiyo mikubwa barani Afrika, ambapo timu hiyo ilimaliza safari yake katika hatua ya makundi kabla ya kurejea nyumbani.

Baada ya kumalizika kwa majukumu ya kimataifa, mshambuliaji huyo ameungana tena na kikosi cha Simba na tayari ameanza mazoezi, akionyesha utayari wake wa kurejea katika ushindani wa klabu.

Mukwala ni miongoni mwa wachezaji waliofanya mazoezi ya mwisho kwenye Viwanja vya Maisara, kisiwani Unguja, kama sehemu ya maandalizi ya mechi ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi 2026.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa leo Alhamisi Januari 8, 2026 katika Uwanja wa New Amaan Complex, kuanzia saa 2:15 usiku, ambapo Simba itakutana na wapinzani wao Azam FC.

Kurejea kwa Mukwala kunampa chaguo zaidi Kocha Mkuu Steve Barker, huku kukitarajiwa kuongeza uimara na ushindani katika safu ya ushambuliaji wa Simba kuelekea mchezo huo muhimu wa kusaka tiketi ya fainali.

The post MUKWALA AONGEZA NGUVU KUELEKEA NUSU FAINALI appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post Wakazi wa Lindi Waendelea kusherehekea Mwaka Mpya na Makapu ya Vodacom
Next Post DAMARO, MAROUF KUIKABILI SINGIDA NUSU FAINALI
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook