Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

TPSF Kuongoza Uwekezaji Utakaozalisha Maelfu ya Ajira

  • 50
Scroll Down To Discover

TPSF kuongoza uwekezaji utakaozalisha maelfu ya ajira

Shirikisho la Sekta Binafsi Tanzania TPSF limepanga kuhamasisha uwekezaji kwa kiwango kikubwa ili kupanua biashara zao kwa lengo la kuongeza uzalishaji kuendana na mabadiliko ya teknolojia huku ikizalisha mamilioni ya ajira kwa Watanzania.

Rais wa TPSF Angelina Ngalula amesema hayo wakati wa hafla ya kujenga na kuimarisha mahusiano kati ya sekta binafsi na wanachama wake ambapo ameeleza namna taasisi hiyo inavyo endeleza jukumu la kuchangia mageuzi ya kiuchumi.

Amesema Shirikisho hilo lina nafasi ya kuendelea kuwa sehemu ya taasisi kiunganishi katika ukuaji wa uchumi wa Taifa kwa kuendelea kufanya uwekezaji kwenye maeneo tofauti ambayo Serikali imefungua mianya kwa wawekezaji kuwekeza.

Serikali kupitia kwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga imewahakikishia wawekezaji juu ya azma ya dhati ya serikali kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji, uendelevu wa viwanda kwa lengo la kufikia uchumi wa kati wa uchumi,

Naye Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mahmoud Thabit Kombo kwa upande wake amesema sekta ya serikali ndio injini ya kuukwamua uchumi wa nchi kutoka hapa ulipo kwenda hatua nyingine hivyo ushirikiano wao na serikali ndio utakayofanya malengo hayo yatimie.

David Silinde Naibu Waziri wa Kilimo nae akabainisha malengo ambayo sekta yake imepanga kuyafikia ikiwemo kuwa na kilimo cha uhakika cha umwagiliaji.

“Hadi kufikia mwaka 2050 tumepanga kuzifikia hekta Milioni nane nchini, tunatoa mwanya kwa wawekezaji nchini kuja kuwekeza kwenye sekta ya umwagiliaji na zana za kilimo ikiwemo upatikanaji mashine za umwagiliaji ili wakulima wafanye kilimo chenye tija,” amesema Silinde.

 

The post TPSF Kuongoza Uwekezaji Utakaozalisha Maelfu ya Ajira appeared first on Global Publishers.



Prev Post Afrika Kusini Yalaani Hatua ya Trump Kutaka Kuiweka Kando Kutoka G20 2026
Next Post Waziri Kikwete Asisitiza Uweledi na Uwajibikaji kwa Wahitimu wa Chuo cha Utumishi wa Umma
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook