

Polisi Nchini limetoa tahadhari kali kwa makundi na watu binafsi wanaotoa kauli, matangazo au mikutano inayoweza kuhatarisha amani na kuibua chuki miongoni mwa Wananchi, likisisitiza kuwa halitasita kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria.
Katika taarifa iliyotolewa leo Novemba 21,2025 na Msemaji wa Jeshi la Polisi kutoka Makao Makuu ya Polisi jijini Dodoma, jeshi hilo limesema linaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa hali ya usalama nchini, hususan katika kipindi hiki ambacho kumeshuhudiwa ongezeko la matamko yanayodaiwa kuashiria kuvuruga utulivu wa nchi.












Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!