

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema imefuatilia makala iliyochapishwa muda mfupi uliopita na chombo cha habari cha CNN kuhusu matukio ya tarehe 29 Oktoba, 2025 na siku zilizofuata.
Taarifa ya leo Novemba 21, 2025 iliyotolewa na Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa imesema “Tunachambua na kuhakiki maudhui yaliyomo katika makala hiyo na tamko la Serikali litakuja baada ya kukamilika kwa uhakiki huo.”

Mapema leo Novemba 21, 2025, CNN ilitoa ripoti ya uchunguzi wake wa kina ambapo imedai imebaini ushahidi unaoonyesha kuwa Polisi wa Tanzania walitumia risasi kuwashambulia na kuwaua waandamanaji waliokuwa wakipinga Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29.
Ripoti hiyo ya CNN ikiongozwa na mwandishi Larry Madowo imedai imeufanya uchunguzi huo kwa uchambuzi wa forensic, ikiwemo muunganiko wa video, picha za maeneo ya tukio, na picha za satelaiti.












Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!