Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Hii Hapa Orodha ya Washindi wa Tuzo za CAF 2025 Zilizofanyika Morocco

  • 14
Scroll Down To Discover

Sherehe za utoaji wa Tuzo za Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF Awards 2025) zimefanyika kwa kishindo na kushuhudia wachezaji, makocha, marefa na timu mbalimbali zikitambuliwa kwa mafanikio ya mwaka. Mwaka huu Morocco imeendelea kung’ara kwa namna ya kipekee katika tuzo nyingi, huku Afrika Mashariki pia ikipata mwakilishi kupitia bao la mwaka.

Washindi wa Tuzo za Wanaume (Men’s Categories)

🔹 Mchezaji Bora wa Mwaka Afrika – Achraf Hakimi (Morocco / PSG)
Beki mahiri wa Morocco amefanikiwa kutwaa tuzo ya juu kabisa akivuna matunda ya msimu wenye mafanikio makubwa.

🔹 Kipa Bora wa Mwaka – Yassine Bounou (Morocco / Al Hilal)
“Bono” ameendelea kuthibitisha ubora wake kama mmoja wa makipa bora duniani.

🔹 Mchezaji Chipukizi wa Mwaka – Othmane Maamma (Morocco / Watford)
Kijana huyu amekuwa gumzo kutokana na kasi ya kukuwa kwake katika soka la Ulaya.

🔹 Mchezaji Bora wa Klabu – Fiston Mayele (DR Congo / Pyramids FC)
Aliyekuwa nyota wa Yanga SC ametwaa tuzo kubwa sana katika ngazi ya vilabu barani Afrika.

🔹 Kocha Bora wa Mwaka – Bubista (Cape Verde)
Amepokea tuzo hii baada ya kuiongoza Cape Verde kufanya makubwa kwenye michuano ya kimataifa.

🔹 Timu Bora ya Taifa ya Mwaka – Morocco U20
Vijana hawa wameipatia nchi yao heshima kubwa kwa mafanikio makubwa katika mashindano ya vijana.

🔹 Klabu Bora ya Mwaka – Pyramids FC (Egypt)
Baada ya uwekezaji mkubwa, Pyramids FC sasa imeanza kuona matunda yob ndani ya bara.

Washindi wa Tuzo za Wanawake (Women’s Categories)

🔹 Mchezaji Bora wa Mwaka – Ghizlane Chebbak (Morocco / Al Hilal)
Nyota huyu ameendelea kutawala soka la wanawake Afrika kwa ubora wa juu kila msimu.

🔹 Kipa Bora wa Mwaka – Chiamaka Nnadozie (Nigeria / Brighton)
Nnadozie ameweka historia kwa kutwaa tuzo hii kwa mara ya tatu mfululizo.

🔹 Mchezaji Chipukizi wa Mwaka – Doha El Madani (Morocco / AS FAR)
Kipaji kipya kinachokuja kwa kasi kutoka AS FAR.

🔹 Timu Bora ya Taifa ya Mwaka – Nigeria (Super Falcons)
Timu yenye historia kubwa imeendelea kulinda hadhi yake barani Afrika.

Tuzo za Waamuzi na Makundi Mengine

🔹 Refa Bora wa Mwaka (Wanaume) – Omar Abdulkadir (Somalia)
🔹 Msaidizi Refa Bora (Wanaume) – Liban Abdoulrazack (Djibouti)
🔹 Refa Bora wa Mwaka (Wanawake) – Samirah Nabadda (Uganda)
🔹 Msaidizi Refa Bora (Wanawake) – Tabara Mbodji (Senegal)

Tuzo Maalum – Bao Bora la Mwaka

Clement Mzize (Young Africans SC – Tanzania)
Mzize ameiletea Tanzania heshima kubwa kwa kutwaa tuzo ya “Goal of the Year” kupitia bao lake maridadi lililovutia bara zima.



Prev Post Wasaidizi 9 wa Familia ya Bongo Wahukumiwa Kwa Ufujaji wa Fedha za Umma
Next Post Tanzania Yapokea Mabaki ya Joshua Mollel Aliyeuawa na Hamas, Mazishi Kufanyika leo Manyara
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook