

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema moja ya mambo yanayotarajiwa kuchunguzwa Tume Huru ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyotokea Oktoba 29, 2025 ni pamoja na kuchunguza haki ambayo ilikua inadaiwa na vijana walioandamana ni ipi hasa.
“tume tunaitarajia ikatuangalizie sababu hasa iliyoleta kadhia ile sababu hasa ni nini, chanzo cha tatizo nini”
Ameongeza akisema “vijana waliingizwa barabarani kudai haki tunataka kujua haki gani vijana hawa wameikosa ili tuweze kuifanyia kazi wapate haki yao”Akizungumza Ikulu Chamwino, Dodoma, Novemba 20, 2025 wakati wa uzinduzi wa tume hiyo, Rais Samia ameitaka Tume hiyo kutazama sura nzima ya mgogoro, ikiwemo mitazamo, tamko na hatua za wadau wote.
Amesema madai haya, iwapo ni ya kweli, yana uzito ambao unahitaji kuchunguzwa kwa undani ili taifa lipate majibu sahihi na hatua stahiki zichukuliwe.
Rais amesisitiza kuwa hata kama kulikuwa na changamoto za kisiasa kati ya vyama, Tume ya Uchaguzi, Msajili wa Vyama au Serikali, haipaswi kufikia hatua ya vurugu, uharibifu na vifo.
Rais pia ametaka tume ichunguze kauli zilizokuwa zikitolewa na baadhi ya makundi wakati wa vurugu, ikiwemo madai ya kutaka Tanzania kufuata mkondo uliotokea Madagascar.
Stori na Elvan Stambuli – Global Publishers











Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!