Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Waendesha Bodaboda Watakiwa Kuepuka Vitendo Vya Uhalifu

  • 24
Scroll Down To Discover

Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita limewataka maafisa usafirishaji (bodaboda) kujiepusha na vitendo vyovyote vya uhalifu au uvunjifu wa amani kutokana na makundi yenye nia ovu kudaiwa kuwashirikisha baadhi ya vijana wakiwemo waendesha bodaboda katika vitendo vya kihalifu.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Operesheni Mkoa wa Geita, ACP Amon Challe Mimata, katika kikao kazi cha wadau wa usafirishaji kwa kutumia pikipiki kilichofanyika Novemba 15, 2025 katika Bwalo la Polisi mkoani humo.

ACP Mimata amewataka waendesha bodaboda kutokubali kushawishiwa au kuhusishwa na vikundi vya kihalifu vinavyohamasisha vurugu au vitendo vyovyote vinavyoweza kuhatarisha amani na utulivu katika mkoa wa Geita. Aidha, amewataka waendesha bodaboda kutoa taarifa mapema pindi wanapobaini dalili, mipango au mikusanyiko ya watu wenye nia ovu ya kuvuruga amani na utulivu

“Kamwe msikubaliane na watu wenye nia ovu. Mkiona dalili za mipango ya uvunjifu wa amani, msitazame tu, hata kama ni ndugu yako, toa taarifa mara moja kwa Jeshi la Polisi mapema ili hatua zichukuliwe” amesema ACP Mimata.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Waendesha Bodaboda Mkoa wa Geita, Fred Fideli, ameshukuru Jeshi la Polisi kwa kutoa elimu hii muhimu huku akiahidi kuwasimamia maafisa usafirishaji kuzingatia sheria na kuendeleza ushirikiano na Jeshi la Polisi katika kuhakikisha jamii inakuwa na amani na usalama.



Prev Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 17, 2025
Next Post Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba Akabidhiwa Ofisi na Kassim Majaliwa
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook