

Jana jumamosi Tarehe 16 , Chuo cha Mamdogo Beauty Training Center kilichopo Kimara, Dar es Salaam, kimefanya mahafali ya wanafunzi waliohitimu mafunzo ya urembo, ambapo zaidi ya wanafunzi mia moja wamekamilisha rasmi masomo yao.
Mgeni rasmi wa mahafali haya alikuwa mwanamitindo Jasinta Makwabe, ambaye alitoa hotuba yenye maadili na hamasa kwa wahitimu. Jasinta aliwakumbusha mabinti kuwa mwanamke anapaswa kusimama imara, kufuatilia ndoto zake na kupigania kile anachokiamini, bila kutegemea msaada wa wanaume katika kila jambo. Alisisitiza umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii, kujitegemea kiuchumi na kujenga maisha yenye mwelekeo na thamani.

Aidha, Jasinta alikisifu Chuo cha Mamdogo Beauty Training Center kwa kuwa chombo muhimu katika kuwawezesha mabinti na wanawake vijana, kimekuwa msaada mkubwa kwa miaka mingi katika kuwaondoa mitaani na majumbani bila mwelekeo, na kuwapatia ujuzi wa urembo unaowawezesha kujipatia kipato halali na kujitegemea.
Mmiliki wa chuo hicho alitoa salamu za pongezi na ushauri kwa wahitimu, akiwataka kutumia ujuzi waliopata kwa manufaa yao na ya jamii.
Chuo cha Mamdogo Beauty Training Center kimejipambanua kama kituo mahiri cha kuwaandaa wataalamu wa urembo, kikitoa mafunzo ya ususi, make-up, skincare, nails, pamoja na upambaji wa maharusi. Kupitia mafunzo ya vitendo na stadi za biashara, chuo hiki kimekuwa msaada mkubwa kwa mabinti wanaotaka kujitegemea. Mawasiliano: 0719 569 760.











Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!