Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Video: Rais Samia Awapa Pole Waathiriwa wa Vurugu, Aahidi Hatua Madhubuti

  • 11
Scroll Down To Discover

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema taifa linapitia kipindi kigumu kutokana na vifo na uharibifu wa mali vilivyoripotiwa katika vurugu za siku ya uchaguzi Oktoba 29, 2025, na kwamba hatua za msingi zimeanza kuchukuliwa ili kurejesha maelewano na amani.

Akizungumza Ijumaa, Novemba 14, 2025, wakati akilifungua Bunge la 13 jijini Dodoma, Rais Samia ameanza hotuba yake kwa kuwataka wabunge na wageni kusimama kwa dakika moja kuwaombea watu waliopoteza maisha.

Rais Samia ameongeza kuwa amehuzunishwa binafsi na matukio hayo, akitoa pole kwa familia zilizoondokewa na wapendwa wao, majeruhi na wale walioathiriwa kwa uharibifu wa mali.

Ameeleza kuwa Serikali tayari imeunda Tume inayochunguza chanzo na mtiririko wa matukio hayo, ili kutoa mwongozo wa hatua zitakazosaidia kurejesha utulivu.



Prev Post Rais Samia Aagiza Vijana Waliofuata Mkumbo Katika Maandamano Kuachiwa Huru – Video
Next Post Vibonge Kunyimwa Visa? Haya Ndiyo Mapya Kutoka Serikali ya Rais Trump
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook