Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Denmark Kupiga Marufuku Mitandao ya Kijamii kwa Watoto Chini ya Miaka 15

  • 4
Scroll Down To Discover

Waziri Mkuu Mette Frederiksen

Serikali ya Denmark imetangaza mpango wa kupiga marufuku matumizi ya mitandao ya kijamii kwa watoto walio na umri chini ya miaka 15, ikiwa ni hatua ya kulinda afya ya akili na ustawi wa vijana.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi, marufuku hiyo itaruhusu wazazi kutoa kibali maalum kwa vijana wenye umri kuanzia miaka 13 kutumia baadhi ya majukwaa, chini ya uangalizi maalum.

Hatua hii inafuatia wito wa Waziri Mkuu Mette Frederiksen, alioutoa mwezi uliopita katika hotuba ya ufunguzi wa Bunge, akitaka kuwepo kwa udhibiti mkali wa matumizi ya mitandao ya kijamii kwa watoto kutokana na madhara yake ya kisaikolojia.

“Mitandao hii ya kijamii inastawi kwa kuiba muda wa watoto wetu, utoto wao, na ustawi wao — na sasa tunaweka kikomo kwa hilo,” alisema Waziri wa Kidigitali Caroline Stage Olsen.

Wabunge wengi wameonyesha kuunga mkono pendekezo hilo, na kura rasmi inatarajiwa kupigwa hivi karibuni.

Serikali imebainisha kuwa majukwaa yanayotumiwa zaidi na watoto nchini humo ni Snapchat, YouTube, Instagram, na TikTok.

Ripoti ya Mamlaka ya Ushindani na Wateja ya Denmark iliyotolewa Februari mwaka huu inaonyesha kuwa vijana nchini humo hutumia wastani wa saa 2 na dakika 40 kila siku kwenye mitandao ya kijamii, hali inayotajwa kuongeza changamoto za msongo wa mawazo na utegemezi wa kidijitali.



Prev Post Burkina Faso: Daktari Aliyekosoa Rais Traoré Atumwa Vitani Baada ya Kupata Mafunzo ya Kijeshi
Next Post Rais Kagame Akana Madai ya Kumuandaa Mtoto Wake Kurithi Urais
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook