Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

‘MBAPPE’ WA AZAM FC MAMBO NI ‘FULL NONDO’…..

  • 14
Scroll Down To Discover

BAADA ya kuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi miwili akiuguza majeraha ya goti, kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Cheickna Diakite ‘Mbappe’ amerejea mazoezini na yuko tayari kuivaa Namungo.

Diakite, ambaye ni miongoni mwa wachezaji muhimu katika safu ya ushambuliaji ya “Wanalambalamba”, ameonekana akiwa na ari kubwa wakati akiungana na wenzake kwa mara ya kwanza tangu alipoumia mapema msimu huu.

Kurejea kwake kunakuja wakati muafaka, kikosi cha Azam FC kikiwa kimerejea kambini kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Namungo FC, utakaopigwa Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa, mkoani Lindi, siku ya Jumapili, saa 1.00 usiku.

Kurejea kwa Diakite kutaleta chachu mpya kwenye kikosi, hasa katika eneo la kati na mbele ambapo ubunifu wake na kasi vinatajwa kuwa silaha muhimu kwa timu hiyo inayopigania nafasi ya juu kwenye msimamo wa ligi.

Mchezaji huyo aliyejiunga na Azam FC mapema msimu huu akitokea AS Real ya Bamako Mali, bado ana kazi ya kuhakikisha anatafuta namba kwenye kikosi cha kwanza chini ya Kocha Mkuu Frorent Ibenge.

The post ‘MBAPPE’ WA AZAM FC MAMBO NI ‘FULL NONDO’….. appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post KELVIN JOHN TENA…..AKIZINGUA NA HAPA NDIO BASI …
Next Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 09, 2025
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook