Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Rais Samia Apokelewa Kwa Shangwe Ikulu ya Chamwino Baada ya Kuapishwa

  • 19
Scroll Down To Discover

Dodoma, Tanzania – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amepokelewa kwa shangwe na watumishi wa Ofisi ya Rais, Ikulu, alipowasili katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma mara baada ya kuapishwa rasmi kuendelea na majukumu yake ya kuliongoza taifa.

Mhe. Rais Samia aliwasili katika Ikulu hiyo akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa serikali, ambapo alipokelewa kwa heshima kubwa ikiwemo nyimbo za kizalendo na vifijo kutoka kwa watumishi wa Ofisi ya Rais waliokuwa na furaha kumuona kiongozi wao mkuu.

Mara baada ya mapokezi, Mhe. Rais alikutana na watumishi wa Ofisi ya Rais na kuwashukuru kwa kuendelea kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na kujituma katika kulitumikia taifa. Aidha, aliwahimiza kuendelea kushirikiana na Serikali katika kutekeleza miradi ya maendeleo na kuhakikisha huduma bora kwa wananchi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akikabidhiwa nyaraka za kazi kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka mara baada ya kuwasili katika Ofisi yake Ikulu Chamwino, akiwa tayari kuanza rasmi majukumu yake baada ya kuapishwa.

 



Prev Post Chadema Yatoa Taarifa Kuhusu Makamu Mwenyekiti Wao, John Heche
Next Post Rais Dkt. Samia Aapishwa Kuendelea Kuongoza Tanzania
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook