
Jeshi la Polisi mkoani Mara linamshikilia Adili Matayo (31), mlinzi wa kampuni ya ulinzi ya Guard Force, kwa tuhuma za kumjeruhi kwa risasi mwanafunzi Deus Wambehu (16) wa Shule ya Msingi Majimoto.
Tukio hilo lilitokea wakati Adili Matayo alijaribu kuwakamata watu waliovamia mgodi wa dhahabu wa Chang Shen, ambao walikuwa wakijaribu kuiba mawe yanayodhaniwa kuwa dhahabu.
Mwanafunzi Deus Wambehu anaendelea na matibabu katika Kituo cha Afya Iramba, huku uchunguzi wa tukio ukiendelea na Jeshi la Polisi likisisitiza kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mlinzi huyo.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!