

Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Aida Kenani, amemuuliza Waziri Mkuu iwapo Serikali haioni haja ya kukutana na wadau wa uchaguzi ili kusikiliza malalamiko yao na kuchukua hatua stahiki kwa lengo la kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na haki.
Akiuliza Bungeni leo, Aprili 24, 2025, Kenani amesema kumekuwa na tofauti kubwa kati ya idadi ya wananchi wanaojiandikisha katika daftari la wapiga kura na idadi ya wanaojitokeza kupiga kura, hali inayochangiwa na kukosekana kwa imani kwa vyombo vinavyosimamia uchaguzi.
Akijibu swali hilo, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, amesema Serikali itaendelea kuhamasisha wananchi kujiandikisha na kushiriki kikamilifu katika uchaguzi ili kutimiza wajibu wao wa kidemokrasia.
Ameongeza kuwa Serikali itahakikisha mazingira salama na tulivu wakati wa uchaguzi kwa kufuata maelekezo ya Tume Huru ya Uchaguzi.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!