Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Kesi ya Jinai Dhidi ya Vigogo wa CHADEMA Kuendelea Mahakama Kuu Leo

  • 4
Scroll Down To Discover

Kesi ya jinai namba 48250 ya mwaka 2025 iliyofunguliwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, Said Issa Mohamed, na wenzake wawili Ahmed Rashid Khamis na Maulidah Anna Komu dhidi ya vigogo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), inaendelea leo Jumanne, Oktoba 28, 2025, katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam.

Kesi hiyo, ambayo imefunguliwa kwa hati ya dharura, inaendelea kwa ajili ya kusikilizwa mapingamizi yaliyowasilishwa na upande wa wajibu maombi, sambamba na kuanza kusikilizwa kwa kesi ya msingi.

Taarifa zinaeleza kuwa kesi hiyo inasikilizwa chini ya Jaji Awamu Mbagwa, huku washtakiwa wakuu wakiwa ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara John Wegesa Heche, Katibu Mkuu John Mnyika, Brenda Rupia, Rose Mayemba, Gervas Lyenda, Twaha Mwaipaya, Hilda Newton, pamoja na Bodi ya Wadhamini wa CHADEMA.

Viongozi hao wanadaiwa kukosa kutii amri ya Mahakama Kuu iliyotolewa tarehe Juni 10, 2025, ikiwazuia kujihusisha na shughuli zozote za kisiasa au kiutendaji kwa mwavuli wa CHADEMA hadi uamuzi wa kesi ya msingi utakapotolewa.

Ikumbukwe kuwa, amri hiyo ilitokana na kesi ya madai iliyofunguliwa na Said Issa Mohamed na wenzake dhidi ya Katibu Mkuu na Bodi ya Wadhamini wa CHADEMA, chini ya usikilizwaji wa Jaji Hamidu Mwanga.

Mahakama inatarajiwa kutoa uamuzi juu ya mapingamizi hayo kabla ya kuendelea na usikilizaji wa hoja za msingi katika siku zijazo.

POLISI WATAJA SABABU za KUKAMATWA kwa NIFFER-TUHUMA NZITO za KUCHOCHEA VURUGU KUELEKEA UCHAGUZI MKUU



Prev Post Doreen Peter Noni: Watanzania tumchague Rais Samia, Nchimbi, Wabunge, Madiwani kwa maendeleo ya nchi
Next Post Polisi Yataja Sababu ya Kumkamata Niffer – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook