Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Watu 27 wauawa katika shambulio la kigaidi msikitini Nigeria

  • 45
Scroll Down To Discover

Watu 27 wauawa katika shambulio la kigaidi msikitini Nigeria
Magaidi waliokuwa na silaha jana Jumanne waliwauwa waumini karibu 27 waliokuwa msikitini katika jimbo la Katsina kaskazini magharibi mwa Nigeria.

Taarifa iliyotolewa na Dr. Nasir Muazu Kamishna wa Usalama wa Ndani na Masuala ya Jimbo la Katsina imeeleza kuwa magaidi hao wanaojulikana kama majambazi walifanya shambulizi wakati waumini wa Kiislamu wa jimbo hilo walipokuwa msikitini katika Swala ya Alfajiri.

Muazu amesema kuwa shambulio hilo lilikuwa la kulipiza kisasi kwa hatua iliyochukuliwa na wenyeji wa eneo hilo siku mbili zilizopita. Wakazi wa Unguwan Mantau waliwavizia magaidi na kuua idadi kubwa ya majambazi.

Hadi sasa hakuna kundi lililotangaza kuhusika na hujuma hiyo ya kigaidi msikitini.

Majambazi nchini Nigeria wamekuwa wakivamia vijiji na kuwavizia watu katika barabara kuu nchini humo.

Serikali ya jimbo la Katsina kwa upande wake imeeleza kuwa askari jeshi wa ulinzi na usalama tayari wamefika katika eneo la tukio ili kudumisha amani na utulivu.

Taarifa ya uongozi wa serikali ya Jimbo la Katsina imeeleza kuwa: “Tunafanya kazi ya kuwanasa majambazi wote. Kama serikali, tunapongeza kitendo cha kishujaa cha watu wa Unguwar Mantau, na tumejitolea kupambana na majambazi na kuhakikisha usalama unakuwepo katika jamii zetu zote”.



Prev Post Kashera: Watumishi wa Serikali Kufichua Siri ni Kosa la Jinai
Next Post Dk Biteko Kuzindua Telnolojia ya Kuondoa Uvimbe Bila Upasuaji
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook