Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Rais Samia Aidhinisha 29 Oktoba 2025 Kama Siku ya Mapumziko Taifa

  • 24
Scroll Down To Discover

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutumia mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya Sikukuu za Kitaifa Sura 35, ameidhinisha tarehe 29 Oktoba, 2025 kuwa siku ya mapumziko.

Kufuatia taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka imeeleza kuwa Uamuzi huo umefanyika kwa madhumuni ya kuwawezesha wananchi wenye sifa stahiki wakiwemo watumishi wa umma na wafanyakazi katika sekta binafsi kutumia haki yao ya kikatiba ya kupiga kura.

Kama inavyofahamika, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza siku ya Jumatano tarehe 29 Oktoba, 2025 kuwa siku ya kupiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2025.



Prev Post Uchumi wa Tanzania Umezidi Kuimarika Katika Kipindi cha Miaka Minne Iliyopita
Next Post Mmisionari wa Kimarekani Atekwa Nyara Jijini Niamey, Niger
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook