Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

TRC: Ajali Imesababishwa Na Hitilafu Za Kiundeshaji

  • 48
Scroll Down To Discover

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetoa taarifa kwa umma kuhusu ajali iliyohusisha treni ya EMU iliyokuwa ikisafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma majira ya saa 2:00 asubuhi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ajali imetokana na hitilafu za kiutendaji ambazo zilisababisha mabehewa matatu ya treni hiyo kuacha njia katika kituo cha Ruvu. TRC imethibitisha kuwa hakuna tukio lolote la vifo lililoripotiwa kufikia sasa.

Timu ya wataalamu ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TRC, vyombo vya ulinzi na usalama, na menejimenti ya shirika hilo, inaendelea na uchunguzi wa kina kuhusu chanzo cha ajali hiyo.

TRC imewahakikishia wananchi kuwa juhudi zinaendelea kuhakikisha huduma za reli zinarejea haraka.

Shirika hilo pia limeomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza kufuatia tukio hilo.



Prev Post Amani Golugwa: Tumeuliza Polisi na Uhamiaji, Heche Hajaonekana Tarime – Video
Next Post Serikali Yaongeza Mikopo kwa Wanafunzi, Kafulila Afafanua
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook