MAGAZETI ya Leo Alhamisi 17 April 2025
Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Musukuma amemshauri Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohammed Mchengerwa kuwapima wateule wa Rais wanaotaka kugombea ubunge kabla ya kuruhusiwa.
Ameyasema hayo, Jumatano ya Aprili 15, 2025 bungeni alipokuwa akichangia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2025/26 ya Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).
Mzizi wa hoja ya Musukuma ni kukazia kauli wa Rais Samia Suluhu Hassan aliyoitoa Machi 11, 2025 akiwataka wakuu wa wilaya (DC), wakurugenzi wa halmashauri (DED) na watumishi wengine wa Serikali wanaotaka kujitosa katika Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu kutoa taarifa mapema, la sivyo watakosa vyote.
“Kwa wale wanaotaka kugombea kutokea huko (wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi), natamani CAG (Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali) awafanyie ukaguzi maalumu ili waje humu wakiwa wasafi. Tusiifanye nyumba hii kama kinga,”amesema Musukuma.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!