Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mwili wa Hayati Raila Odinga Wazikwa Kwa Heshima Kuu Siaya – Video

  • 16
Scroll Down To Discover

Mwili wa Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Hayati Raila Amolo Odinga, umezikwa leo katika makazi yake ya nyumbani, Kang’oka Ka Jaramogi, Kaunti ya Siaya.

Mazishi hayo ya kitaifa yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya nchi, wakiongozwa na Rais wa Kenya, maafisa wa serikali, viongozi wa upinzani, na wawakilishi wa mataifa rafiki.

Baada ya kushushwa kwa jeneza, mizinga 17 ya heshima ilipigwa kwa ajili ya kumuenzi Hayati Raila Odinga — ishara ya heshima kwa wadhifa aliowahi kushika kama Waziri Mkuu na mchango mkubwa alioutoa katika historia ya kisiasa ya Kenya.

Raila Odinga anakumbukwa kama mwanademokrasia, mpigania haki, na kiongozi aliyejitolea kwa maendeleo ya taifa lake.



Prev Post Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 19, 2025
Next Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO OKTOBA 20, 2025
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook