Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Kesi ya Uhaini ya Tundu Lissu Yaahirishwa Ili Shahidi Atumie Kompyuta Kutambua Vielelezo

  • 15
Scroll Down To Discover

Kesi ya Uhaini inayomhusu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu imeahirishwa kwa muda mpaka saa tisa kamili Alasiri baada ya Mahakama kutaka shahidi apate kompyuta itakayomuwezesha kutambua kama vielelezo alivyokabidhiwa ni sahihi.

Hii inakuja baada shahidi huyo kukukabidhiwa bahasha na Wakili wa Serikali Mkuu Thawabu Issa inayodaiwa kuwa na vielelezo viwili ambavyo ni flash disc ya GB 8 na Memory card ya Aldeepo yenye GB 32.

Katika maelezo yake shahidi wa tatu wa Jamhuri Samweli Elibariki Kaaya ambaye ni Mkaguzi wa Jeshi la Polisi aliieleza mahakama kuwa April 8, 2025 alikabidhi kwa ASP Michael Gyumi bahasha ambayo ilikuwa na vielelezo hivyo.

Hata hivyo alivyoonyeshwa bahasha hiyo leo mahakamani na Wakili wa Serikali Mkuu Thawabu Issa alikiri kuwa ndiyo aliyokabidhi kwa ASP Gyumi kwani ameitambua kwa uwepo wa mhuri wa Jeshi la Polisi, Majina na saini yake, Vielelezo viwili pamoja na ‘evidence tape’.

Katika kuhitaji kuhakikisha vilivyomo ndani ya vielelezo hivyo ndipo ilipoibuka hoja kutoka kwa Lissu akihitaji itumike kompyuta au laptop kutoka kwa Mawakili wa Serikali.

Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar Es Salaam imeahirisha kesi kwa lisaa limoja na nusu mpaka saa tisa kamili(kuanzia saa saba na nusu) ili shahidi apate kompyuta maalum kwa ajili ya shahidi kuweza kutambua ushahidi ulio kwenye flash disc na memory card kama ndio wenyewe au lah.

WAKENYA WAMPIGIA SHANGWE UHURU KENYATTA MSIBANI KWA RAILA ODINGA – ”NILIMPENDA KAMA NDUGU YANGU”



Prev Post Makamu wa Rais Dkt. Mpango Atoa Heshima za Mwisho kwa Raila Odinga Jijini Nairobi
Next Post Dkt. Philip Mpango Awasili Nairobi Kumuwakilisha Rais Samia katika Mazishi ya Raila Odinga
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook