
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango, ametoa heshima za mwisho kwa mwili wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya, marehemu Raila Amolo Odinga, katika Mazishi ya Kitaifa yaliyofanyika leo, tarehe 17 Oktoba 2025, katika Uwanja wa Nyayo, jijini Nairobi, Kenya.
Dkt. Mpango alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwenye tukio hilo ambalo limehudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wa kitaifa na kimataifa waliokuja kutoa heshima zao za mwisho kwa kiongozi huyo mkongwe wa siasa za Kenya na Afrika Mashariki.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!