Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mkulima Singida Ahukumiwa Kifungo cha Maisha kwa Kumbaka Mjukuu Wake

  • 16
Scroll Down To Discover

Mahakama ya Wilaya ya Singida imemhukumu Hamis Said Debwa (65), mkulima na mkazi wa Mnung’una, kifungo cha maisha jela kwa kosa la ulawiti na kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kuzini na maharimu.

Mshitakiwa alitenda makosa hayo Januari 19, 2025 katika kijiji cha Minga, Kata ya Unyamkumi, kwa kumbaka na kumlawiti mjukuu wake mwenye umri wa miaka 7. Alikamatwa na Jeshi la Polisi na kufikishwa mahakamani Januari 29, 2025.

Hukumu hiyo imetolewa Oktoba 15, 2025 na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Singida, Mhe. Fadhili Luvinga, ambaye amesema adhabu hiyo inalenga kutoa fundisho kwa wengine na kusaidia kuondoa vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii.

SASAMPA YAMGOMBANISHA DIAMOND NA MARIOO? /HARMONIZE AAMUA KUSAMEHE/HUNTER NA RASCO WAFUNGUKA



Prev Post Serikali Yapandisha Kima cha Chini cha Mshahara kwa Sekta Binafsi kwa Asilimia 33.4
Next Post Odinga Alipokutana Live na Mwandishi wa Global na Kumshangaza
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook