Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Serikali Yapandisha Kima cha Chini cha Mshahara kwa Sekta Binafsi kwa Asilimia 33.4

  • 12
Scroll Down To Discover

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Ridhiwan Jakaya Kikwete.

Serikali imetangaza ongezeko la kima cha chini cha mshahara kwa wafanyakazi wa sekta binafsi kwa wastani wa asilimia 33.4, kutoka Sh275,060 hadi Sh358,322 kwa mwezi.

Akizungumza leo Oktoba 17, 2025, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Ridhiwan Jakaya Kikwete, amesema kuwa kima hicho kipya kitaanza kutumika rasmi kuanzia Januari 1, 2026.

Waziri Kikwete amewataka waajiri wote nchini kuzingatia masharti ya sheria za kazi na kuhakikisha wanalipa mishahara kwa mujibu wa kiwango kipya ili kuboresha hali ya maisha ya wafanyakazi.

Aidha, Serikali inaendelea na juhudi za kuimarisha ustawi wa wafanyakazi nchini, ikikumbukwa kuwa awali ilipandisha kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma kwa asilimia 35.1, kutoka Sh370,000 hadi Sh500,000.



Prev Post Vodacom na Bolt kwa Pamoja Kutoa Punguzo kwa Kila Safari Kupitia Tuzo Points
Next Post Mkulima Singida Ahukumiwa Kifungo cha Maisha kwa Kumbaka Mjukuu Wake
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook